Monday, December 30, 2013
OBAMA NA MKEWE MICHELLE WADAIWA KUTENGANA.
RAIS wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle wanadaiwa kutengana. Habari zinadai kuwa wawili hao wanalala katika vyumba tofauti kwa sasa ndani ya Ikulu ya Marekani 'White House'. < Mgogoro baina ya wawili hao ulianza zamani na wameweza kuendelea kuishi pamoja kwa sababu ya watoto wao wawili wa kike Sasha na Malia na kulinda heshim a ya urais.
Michelle anadai amechoka na atakutana na mwanasheria wa masuala ya talaka ili aweze kuachana na rais huyo wa 44 nchini Marekani. Michelle ataendela kuishi Ikulu 'White House' kwa muda wote uliobaki katika kipindi cha utawala wa Obama, ila ameweka wazi kuwa watakuwa wakiishi vyumba tofauti.
Anataka kuishi katika chumba kimojawapo cha familia kilichowazi na anajiandaa kuhamisha nguo zake na kila kilicho chake kutoka kwenye jumba lao la kifahari la mamilioni ya dola lililopo Chicago.
Michelle alichanganyikiwa zaidi baada ya Obama kupiga picha za kimahaba akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya marehemu Nelson Mandela nchini Afrika Kusini.
Obama mwenye miaka 52, alikuwa akifurahi, kunong'enezana na kumshika begani mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Denmark tangu Oktoba 3, 2011
YADAIWA KUACHANA KWA DIAMOND NA PENNY SIO KISA WEMA, NI KIGOGO MMOJA WA CCM, SOMA ZAIDI.
Imebainika kuwa kuvunjika kwa uchumba baina ya Naseeb Abdull 'Diamond' na Penieli Mwigila kumechangiwa na kigogo mmoja wa CCM ambaye amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Penny! Swahilitz inakupa full details
Habari za ndani kutoka vyanzo vyetu zimebainisha kuwa tangu siku nyingi kigogo huyo wa CCM (jina tunalo) amekuwa akilifaidi penzi la mwanadada Penny kwakuwa anamkono wa birika (mgumu kwenye fedha) licha ya kwamba fedha anazo.
Akitoboa siri za ndani, mnyetishaji wetu amesema kwamba mbali ya ubahili wa Diamond pia ndugu wa upande wa Penny hawakuwa wakipenda binti yao aishi na Diamond kwa kuwa hana sifa za kuishi naye hali iliyo mrahisishia kigogo huyo kula vya watu
Kikaongeza "Hata kuachana kwao ni Penny ndiye aliyemuacha Diamond kwa sababu ambazo si za msingi sana kwani siku nyingi Penny alishakata tamaa ya kuishi na Diamond
"Nakumbuka kipindi baba yake Wema alipofarikil, Diamond alitaka kwenda msibani kuzika lakini alikuwa anashindwa atamuagaje Penny, hivyo akaamua amsukumizie mzigo Babu Tale ili ampigie simu na kujifanya yeye ndiye aliyemshinikiza kwenda kuzika"
"Sasa siku Diamond alipoaga kwenda Msibani, Penny 'akamtaiti' na kumuuliza anakwenda kumzika nani? Diamond akamwambia amuulize Babu Tale lakini Penny alimgomea na kumwambia wewe ndiye unayekwenda kuzika na wewe ndiye unayenihusu nitamuuliza vipi Babu Tale?
"Diamond akawa hana cha kujibu zaidi ya kuzuga kisha baadae kuondoka na kwenda Zanzibar kuzika" kilisema chanzo hicho
Hata hivyo habri zaidi zinasema kabla ya Bifu hilo halijatokea Diamondi alikuwa amesha mpatia kiasi cha fedha Penny kwa ajili kutafuta nyumba akapange ili waishi tofauti na familia jambo ambalo Diamond aligomea kipindi alipokuwa akiishi na Wema.
"Kwa hiyo Diamond alipoondoka tu kwenda Zanzibar, Penny naye akahama nyumbani kwao akawa anaishi kwenye hotel moja Sinza, wakati mwingine alikuwa akionekana hotelini hapo na wifi yake, kipindi hicho ndipo kigogo wa CCM naye akajitanua zaidi na kuanza kumuhudumia Penny kama mkewe.
"Licha ya kwamba mama na dada wa Diamond walikuwa wakimkubali sana Penny na kujaribu kumsihi kutomwacha kijana wao lakini Penny alishakuwa ameonyesha Dalili zote za kutoishio nyumbani kwa mama Naseeb"
Kipindi Fulani Diamond alijaribu kubembeleza uchumba kwa Penny hadi akauchimba ukoo wao na kugundua kuwa baba yake Penny na Bibi yake Diamond wamewahi kuishi kijiji kimoja (huko kigoma) hivyo Diamind akazusha habari kuwa wao ni Ndugu akiamini itamsaidia kuwafanya wazazi wa Penny anafaa kumuoa binti yao lakini ugunduzi huo ukageuka kuwa kashfa mpya!" kilisema chanzo hicho
"Kimsingi huyo kigogo niliyewatajia ndiye anahudumia Penny , fanyeni utafiti mtagundua" kilimaliza chanzo hicho
Baada ya kupata taarifa hizo Swahilitz ilimpigia Simu Penny ili kuweka sawa taarifa hizi lakini iliita bila kupokelewa.
Jitihada za kumhoji kigogo huyo zinaendelea
Saturday, December 14, 2013
SOMA HAPA UJUE KWANINI MTANGAZAJI OPRAH WINFREY HANA MTOTO HADI LEO. (MIAKA 59)
Akiwa na umri wa miaka 59, Mtangazaji hodari wa show za mahojiano duniani Oprah Winfrey ambae miezi kadhaa iliyopita aliitembelea Tanzania kwenye mbuga za wanyama, amesema hajutii kutokuwa na watoto maishani mwake.
Oprah ambae aliwahi kubakwa akiwa na umri wa miaka 14 na kujifungua mtoto ambae hata hivyo alifariki dunia siku chache baada ya kuzaliwa, anaamini kama angekuwa mama maisha yake ya kazi yangeingiliana na maisha yake ya familia .
Anakwambia ‘kama ningekuwa na watoto kwa hakika watoto hawa wangenichukia, wasingeweza kunipenda kwa kuwa wangeingia kwenye ushindani na kazi yangu, wangekuwa kama watu wengi mnaowaona kwenye show zangu wakizungumzia familia zao kutokuwa na mapenzi na watoto wao, maishani mwao wangekosa kitu muhimu ambacho ni upendo wa mama’
SOMA HAPA NA USIKILIZE U-HEARD YA JUZI BAADA YA LULU NA YOUNG DEE KUKUTWA NDANI YA GARI USIKU WA MANANE WAKINANIII!!!
kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds FM chini ya bwana Sudi Brown ama Gossip Cop kulikuwa na FUNUNU kali iliyokuwa inamuhusu mwanadada wa bongomovies Elizabeth Bin Michael a.k.a LULU na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Young D al-maarufu kama Young Dar es salaam kama mwenyewe anavyojiita ya wawili hao kukutwa kwenye gari wakifanya lile tendo linaloruhusiwa kufanywa mara baada ya mdada na mkaka kufunga ndoa.
Kwa mujibu wa Sudi Brown = Gossip cop, wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezibeach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada lulu na polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.
Habri zainasema Baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongeana polisi kabla ya wao kutokomea wasipojulikana na gari hilo.
Alipopigiwa simu mwanadada LULU alipokea na kukata muda mfupi na baadaye Young D alipopigiwa simu alitoa majina ya utata kama alivyoongea mwenyewe kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds fm
MSIKILIZE HAPA SUDI BROWN AKIONGEA NAO
https://soundcloud.com/darvel-kardashian-1/lulu-na-young-dee-u-heard-tar
Kwa mujibu wa Sudi Brown = Gossip cop, wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezibeach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada lulu na polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.
Habri zainasema Baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongeana polisi kabla ya wao kutokomea wasipojulikana na gari hilo.
Alipopigiwa simu mwanadada LULU alipokea na kukata muda mfupi na baadaye Young D alipopigiwa simu alitoa majina ya utata kama alivyoongea mwenyewe kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds fm
MSIKILIZE HAPA SUDI BROWN AKIONGEA NAO
https://soundcloud.com/darvel-kardashian-1/lulu-na-young-dee-u-heard-tar
Saturday, December 7, 2013
Filamu ya Fast and Furious 7 itachelewa kutoka mapema sababu ya kifo cha Paul Walker
Kabla ya kifo cha Paul Walker cast na crew nzima walikuwa wameshapanga bajeti kwaajili ya kusafiri kuelekea Abu Dhabi mnamo mwezi January 2014 kushooting baadhi ya scenes
Cast pamoja na crew ilipumzika kwa muda ili kupisha sikukuu za marekani 'Thanks Giving' lakini walitakiwa kurejea Atlanta siku ya Jumapili kuendelea na scenes kadhaa, ambapo ndipo mwenzao Paul Walker akawa amekumbwa na mauti baada ya kugonga mti na kupata ajali ya gari.
Waandaaji wa filamu hiyo Fast and Furious 'Hurricane Katrina Drama wamesema wataendelea na ratiba ya kuichia rasmi Desemba 13. 'Fast and Furious 7.
Subscribe to:
Posts (Atom)