Wednesday, January 1, 2014

BREAKING NEWS: WAZIRI WA FEDHA DK.WILLIAM MGIMWA AFARIKI DUNIA



Waziri wa Fedha, Dk. William Augustao Mgimwa (63) amefariki dunia.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha Waziri wa Fedha, Mheshimiwa William Mgimwa, aliyekuwa pia Mbunge wa Jimbo la Kalenga (Mkoa wa Iringa) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete amesema kuwa taifa limempoteza Waziri Mgimwa katika kipindi lilipokuwa linamhitaji zaidi kutokana na mchango wake mkubwa ambao amekuwa akiutoa kupitia nafasi zake za Waziri wa Serikali na mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kalenga.
Kifo cha Mheshimiwa Mgimwa kimetangazwa mchana wa leo, Jumatano, Januari Mosi, 2014, na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Sefue kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika tangazo lake, Balozi Sefue amesema kuwa Waziri Mgimwa ameaga dunia asubuhi ya leo saa 5:20 (Saa za Afrika ya Kati) katika Hospitali ya Kloof Medi-Clinic , Pretoria, Afrika Kusini ambako amekuwa amelazwa kwa muda sasa.
Balozi Sefue amesema kuwa maandalizi ya kuurudisha nyumbani mwili wa Waziri Mgimwa yanafanywa na Serikali kwa kushirikiana na familia yake na kuwa taarifa zaidi za suala hilo zitatolewa baadaye kwa kadri zinavyopatikana na maandalizi yanavyoendelea.
Katika salamu zake kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda na kwa familia ya Marehemu Mgimwa, Rais Kikwete amesema:  “Sina maneno ya kutosha kuelezea mshtuko na huzuni yangu kubwa kufuatia taarifa za kifo cha Mheshimiwa Mgimwa.
Binafsi nimemtembelea mara mbili kwenye Hospitali alikokuwa amelazwa na mara ya mwisho hali yake ilikuwa imeimarika. Tulizungumza kwa kiasi cha dakika 10 hivi akanielezea nia yake na tamaa yake ya kurejea nyumbani kwa sababu hali yake ilikuwa nzuri.”
Ameongeza Mheshimiwa Rais Kikwete: “Sote tunajua mchango wake katika Serikali. Sote tulitamani kuendelea kuwa naye, lakini haya ni mapenzi ya Mungu.”
“Napenda kutoa pole nyingi na rambirambi zangu za dhati kwa wana-familia wote kwa kuondokewa na mhimili wao. Naungana nanyi katika kuomboleza msiba huo mkubwa. Napenda mjue kuwa msiba huu ni msiba wangu pia. Machungu yenu ni majonzi yangu,” amesema Rais Kikwete.
Rais pia amewatumia rambirambi wananchi wa Jimbo la Kalenga akisema kuwa wamempoteza mwakilishi na mtetezi mahiri wa maslahi yao.
Mgimwa aliyezaliwa January 20, 1950 na kuwa mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM)
Dk. Mgimwa alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Benki mkoani Mwanza, kabla ya kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Mkoa wa Iringa, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Monday, December 30, 2013

OBAMA NA MKEWE MICHELLE WADAIWA KUTENGANA.


RAIS wa Marekani, Barack Obama na mkewe Michelle wanadaiwa kutengana. Habari zinadai kuwa wawili hao wanalala katika vyumba tofauti kwa sasa ndani ya Ikulu ya Marekani 'White House'. < Mgogoro baina ya wawili hao ulianza zamani na wameweza kuendelea kuishi pamoja kwa sababu ya watoto wao wawili wa kike Sasha na Malia na kulinda heshim a ya urais. 
Michelle anadai amechoka na atakutana na mwanasheria wa masuala ya talaka ili aweze kuachana na rais huyo wa 44 nchini Marekani. Michelle ataendela kuishi Ikulu 'White House' kwa muda wote uliobaki katika kipindi cha utawala wa Obama, ila ameweka wazi kuwa watakuwa wakiishi vyumba tofauti.
Anataka kuishi katika chumba kimojawapo cha familia kilichowazi na anajiandaa kuhamisha nguo zake na kila kilicho chake kutoka kwenye jumba lao la kifahari la mamilioni ya dola lililopo Chicago.
Michelle alichanganyikiwa zaidi baada ya Obama kupiga picha za kimahaba akiwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt, wakati wa mazishi ya marehemu Nelson Mandela nchini Afrika Kusini.
Obama mwenye miaka 52, alikuwa akifurahi, kunong'enezana na kumshika begani mrembo huyo mwenye umri wa miaka 46 ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Denmark tangu Oktoba 3, 2011


YADAIWA KUACHANA KWA DIAMOND NA PENNY SIO KISA WEMA, NI KIGOGO MMOJA WA CCM, SOMA ZAIDI.


Imebainika kuwa kuvunjika kwa uchumba baina ya  Naseeb Abdull 'Diamond' na Penieli Mwigila kumechangiwa na kigogo mmoja wa CCM ambaye amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Penny! Swahilitz inakupa full details

Habari za ndani kutoka vyanzo vyetu zimebainisha kuwa tangu siku nyingi kigogo huyo wa CCM (jina tunalo) amekuwa akilifaidi penzi la mwanadada Penny kwakuwa anamkono wa birika (mgumu kwenye fedha) licha ya kwamba fedha anazo. 

Akitoboa siri za ndani, mnyetishaji wetu amesema kwamba mbali ya ubahili wa Diamond pia ndugu wa upande wa Penny hawakuwa wakipenda binti yao aishi na Diamond kwa kuwa hana sifa za kuishi naye hali iliyo mrahisishia kigogo huyo kula vya watu 

"Amini kwamba katika kipindi chote cha mahusiano yao, Diamond hajawahi kusalimiana na mama yake Penny hata siku moja, hata kaka zake Penny hawataki kabisa kumsikia Diamond na mara kibao wamekuwa wakimsema sana Penny kuhusu Diamond" kimesema chanzo chetu

Kikaongeza "Hata kuachana kwao ni Penny ndiye aliyemuacha Diamond kwa sababu ambazo si za msingi sana kwani siku nyingi Penny alishakata tamaa ya kuishi na Diamond

"Nakumbuka kipindi baba yake Wema alipofarikil, Diamond alitaka kwenda msibani kuzika lakini alikuwa anashindwa atamuagaje Penny, hivyo akaamua amsukumizie mzigo Babu Tale ili ampigie simu na kujifanya yeye ndiye aliyemshinikiza kwenda kuzika"

"Sasa siku Diamond alipoaga kwenda Msibani, Penny 'akamtaiti' na kumuuliza anakwenda kumzika nani? Diamond akamwambia amuulize Babu Tale lakini Penny alimgomea na kumwambia wewe ndiye unayekwenda kuzika na wewe ndiye unayenihusu nitamuuliza vipi Babu Tale?
"Diamond akawa hana cha kujibu zaidi ya kuzuga kisha baadae kuondoka na kwenda Zanzibar kuzika" kilisema chanzo hicho

Hata hivyo habri zaidi zinasema kabla ya Bifu hilo halijatokea Diamondi alikuwa amesha mpatia kiasi cha fedha Penny kwa ajili kutafuta nyumba akapange ili waishi tofauti na familia jambo ambalo Diamond aligomea kipindi alipokuwa akiishi na Wema.

"Kwa hiyo Diamond alipoondoka tu kwenda Zanzibar, Penny naye akahama nyumbani kwao akawa anaishi kwenye hotel moja Sinza, wakati mwingine alikuwa akionekana hotelini hapo na wifi yake, kipindi hicho ndipo kigogo wa CCM naye akajitanua zaidi na kuanza kumuhudumia Penny kama mkewe.

"Licha ya kwamba mama na dada wa Diamond walikuwa wakimkubali sana Penny na kujaribu kumsihi kutomwacha kijana wao lakini Penny alishakuwa ameonyesha Dalili zote za kutoishio nyumbani kwa mama Naseeb"
Kipindi Fulani Diamond alijaribu kubembeleza uchumba kwa Penny hadi akauchimba ukoo wao na kugundua kuwa baba yake Penny na Bibi yake Diamond wamewahi kuishi kijiji kimoja (huko kigoma) hivyo Diamind akazusha habari kuwa wao ni Ndugu akiamini itamsaidia kuwafanya wazazi wa Penny anafaa kumuoa binti yao lakini ugunduzi huo ukageuka kuwa kashfa mpya!" kilisema chanzo hicho

"Kimsingi huyo kigogo niliyewatajia ndiye anahudumia Penny , fanyeni utafiti mtagundua" kilimaliza chanzo hicho

Baada ya kupata taarifa hizo Swahilitz ilimpigia Simu Penny ili kuweka sawa taarifa hizi lakini iliita bila kupokelewa.
Jitihada za kumhoji kigogo huyo zinaendelea

Saturday, December 14, 2013

SOMA HAPA UJUE KWANINI MTANGAZAJI OPRAH WINFREY HANA MTOTO HADI LEO. (MIAKA 59)


Akiwa na umri wa miaka 59, Mtangazaji hodari wa show za mahojiano duniani Oprah Winfrey ambae miezi kadhaa iliyopita aliitembelea Tanzania kwenye mbuga za wanyama, amesema hajutii kutokuwa na watoto maishani mwake.
Oprah ambae aliwahi kubakwa akiwa na umri wa miaka 14 na kujifungua mtoto ambae hata hivyo alifariki dunia siku chache baada ya kuzaliwa,  anaamini kama angekuwa mama maisha yake ya kazi yangeingiliana na maisha yake ya familia .
Anakwambia ‘kama ningekuwa na watoto kwa hakika watoto hawa wangenichukia, wasingeweza kunipenda kwa kuwa wangeingia kwenye ushindani na kazi yangu, wangekuwa kama watu wengi mnaowaona kwenye show zangu wakizungumzia familia zao kutokuwa na mapenzi na watoto wao, maishani mwao wangekosa kitu muhimu ambacho ni upendo wa mama’

SOMA HAPA NA USIKILIZE U-HEARD YA JUZI BAADA YA LULU NA YOUNG DEE KUKUTWA NDANI YA GARI USIKU WA MANANE WAKINANIII!!!

kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds FM chini ya bwana Sudi Brown ama Gossip Cop kulikuwa na FUNUNU kali iliyokuwa inamuhusu mwanadada wa bongomovies Elizabeth Bin Michael a.k.a LULU na mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya Young D al-maarufu kama Young Dar es salaam kama mwenyewe anavyojiita ya wawili hao kukutwa kwenye gari wakifanya lile tendo linaloruhusiwa kufanywa mara baada ya mdada na mkaka kufunga ndoa.
Kwa mujibu wa Sudi Brown = Gossip cop, wawili hao walikutwa maeneo ya Mbezibeach ndani ya gari aina ya Hyundai ya mwanadada lulu na polisi wa doria wakivunja amri hiyo iliyokatazwa na vitabu vyote vitakatifu kwa maana ya biblia, Quran na vitabu vingine vya dini ulimwenguni.
Habri zainasema Baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongeana polisi kabla ya wao kutokomea wasipojulikana na gari hilo.
Alipopigiwa simu mwanadada LULU alipokea na kukata muda mfupi na baadaye Young D alipopigiwa simu alitoa majina ya utata kama alivyoongea mwenyewe kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha clouds fm
MSIKILIZE HAPA SUDI BROWN AKIONGEA NAO
https://soundcloud.com/darvel-kardashian-1/lulu-na-young-dee-u-heard-tar

Saturday, December 7, 2013

New track-Stamina Ft Criss Wamarya - Mngekuwepo ( Digital Vibes )

Filamu ya Fast and Furious 7 itachelewa kutoka mapema sababu ya kifo cha Paul Walker


 Utengenezaji wa filamu mpya ya Fast and Furious  sehemu ya 7 utacheleweshwa kutokana na sababu ya kifo cha mmoja wa mastaa wake, Paul Walker.
Kabla ya kifo cha Paul Walker cast na crew nzima walikuwa wameshapanga bajeti kwaajili ya kusafiri kuelekea Abu Dhabi mnamo mwezi January  2014 kushooting baadhi ya scenes 
 Cast pamoja na crew ilipumzika kwa muda ili kupisha sikukuu za marekani 'Thanks Giving' lakini walitakiwa kurejea Atlanta siku ya Jumapili kuendelea na scenes kadhaa, ambapo ndipo mwenzao Paul Walker akawa amekumbwa na mauti baada ya kugonga mti na kupata ajali ya gari.
Waandaaji wa filamu hiyo Fast and Furious 'Hurricane Katrina Drama wamesema  wataendelea na ratiba ya kuichia rasmi Desemba 13. 'Fast and Furious 7.





LINKwithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...